Binti wa miaka 10 aweka rekodi ya dunia kuandika Riwaya ndefu
Sisti Herman
April 21, 2025
Share :
Binti Hephzibah Akinwale ambaye ni mwandishi wa vitabu raia wa Uingereza na Nigeria mwenye umri wa miaka 10 kutoka Cambridge, Uingereza, ameingia kwenye vitabu vya historia baada ya kuvunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa riwaya ndefu zaidi ya uongo iliyoandikwa na mtoto.
Riwaya yake ya kwanza, Chronicles of the Time Keepers: Whisked Away, ina maneno ya kuvutia 58,000, ikipita rekodi ya awali ya maneno 44,000 iliyokuwa ikishikiliwa na Manikya Sanghi mwenye umri wa miaka 11.