pmbet

Binti wa miaka 16 aokota dhahabu na kuikabidhi polisi

Eric Buyanza

June 30, 2026
Share :

Mwaka 2015 katika mji wa Essen nchini Ujerumani, Binti wa miaka 16 aliyekuwa akiogelea kwenye Ziwa Königssee aliona kitu kinang'aa chini ya maji, baada ya kupiga mbizi aliokota kipande cha dhahabu chenye uzito wa nusu kilo.

 

Dhahabu hiyo ilikuwa na thamani ya karibu Euro 16,000 (sawa na shilingi milioni 47 za Kitanzania).

 

Kwa uaminifu mkubwa Binti akishirikiana na wazazi wake waliamua kuikabidhi dhahabu hiyo mara moja kituo cha polisi cha karibu ambapo mamlaka zilianzisha uchunguzi wa kina uliodumu kwa miezi sita ili kumjua mmiliki halali wa dhahabu hiyo.

Licha ya juhudi hizo hakuna mmiliki yeyote aliyepatikana.

 

Kulingana na sheria za Ujerumani, ikiwa kitu kilichookotwa hakitachukuliwa na mmiliki wake halali ndani ya miezi sita, aliyekipata anakuwa mmiliki rasmi.

Mwaka uliofuata mnamo Februari 2016, mamlaka zilimkabidhi binti huyo dhahabu hiyo kama zawadi ya uaminifu wake na mpaka leo hii bado haijulikani ni nani haswa aliyetupa dhahabu hiyo ziwani na kwa sababu gani.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet