Blobfish ashinda tuzo ya samaki bora wa mwaka
Eric Buyanza
March 19, 2025
Share :
Mara baada ya kutajwa kuwa mnyama anayetisha zaidi duniani kwa mwonekano wake , samaki aina ya blobfish amerejea kwa kishindo: ametangazwa wiki hii kama Samaki bora wa Mwaka na kikundi cha mazingira nchini New Zealand.
Shindano hilo la kila mwaka, linalofanywa na Shirika la Mountain to Sea Conservation Trust, linalenga kuongeza ufahamu wa viumbe vya maji safi na viumbe vya baharini nchini New Zealand.
Samaki huyo aliye na umbo la rojorojo hukua na kufikia urefu wa nchi 12 na hupatikana kwenye kina cha futi 2,000 mpaka 4,000 chini ya bahari.
BBC