Bocco aghairi kustaafu kukiwasha na JKT msimu ujao.
Joyce Shedrack
June 29, 2024
Share :
Aliyekuwa mshambuliaji na Nahodha wa klabu ya Simba John Rafael Bocco huwenda akatimkia JKT Tanzania kama mshambuliaji wao mpya na nahodha wa timu hiyo kuelekea msimu ujao.
Bocco mwenye umri wa miaka 34 hivi karibuni alitangazwa kupewa mkono wa kwaheri na klabu ya Simba akiwa kama mchezji na kutangazwa kugeukia kazi ya ukocha ambapo tayari alikabidhiwa kukinoa kikosi cha Simba chini ya umri wa miaka 17 anatajwa kumalizana na JKT Tanzania akisaini mkataba wa mwaka mmoja akiwa tayari amepiga picha za utambulisho na kaingiziwa pesa zake za usajili.
Mshambuliaji huyo alitangazwa kustaafu kucheza mpira akiwa ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi kwenye Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara baada ya kufunga magoli 155.