Bocco Atambumbulishwa rasmi JKT Tanzania, aanza Mazoezi
Sisti Herman
July 10, 2024
Share :
Klabu ya JKT Tanzania imemtambulisha rasmi aliyekuwa nahodha wa klabu ya Simba, mfungaji bora wa muda wote wa ligi kuu Tanzania na mfungaji bora namba nne wa timu ya Taifa Tanzania "Taifa Stars" John Raphael Bocco kuwa mchezaji wao rasmi.
Bocco ambaye aliagwa na klabu ya Simba na kutambulishwa kuwa kocha wa timu ya vijana ambayo alianza kuifundisha kwa miezi kadhaa amejiunga JKT na tayari ameanza mazoezi na klabu hiyo.