pmbet

Bocco na Simba ndio basi tena

Eric Buyanza

December 8, 2023
Share :

Huenda nyakati za mshambuliaji bora wa muda wote wa Ligi kuu Tanzania bara, John Raphael Bocco zikafikia ukingo dirisha dogo la usajili lijalo baaada ya uongozi wa klabu hiyo kusemekana kumtoa kwenye mipango yao ya msimu ujao.

Simba sasa inajiandaa kuachana na wachezaji wake wasiopungua watano kwenye dirisha dogo hili la usajili huku wengine wakisubiriwa mwisho wa msimu ufike wamalize mikataba yao na kuondoka huru.
 

Taarifa za ndani kutoka kwenye klabu hiyo zimethibitisha kuwa tayari uongozi wa Simba umemalizana na Bocco kwa kumpa uhuru wa kuchagua kuondoka Msimbazi kwenye dirisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa Desemba 16, mwaka huu na kama ikishindikana basi atasubiri hadi mwisho wa msimu mkataba wake umalizike aondoke.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet