pmbet

Bodaboda afariki baada ya kunywa chupa 5 za pombe kali

Eric Buyanza

June 29, 2024
Share :

Dereva bodaboda anayefahamika kwa jina la Charles Ngaga, amefariki dunia usiku wa kuamkia Juni 28, 2024 katika Mtaa wa Kiswanya A, Manispaa ya Morogoro baada ya kushindana na wenzake kunywa pombe kali, chupa tano kwa wakati mmoja, jambo lililosababisha kifo chake.

Baba wa marehemu, John Ngaga amesema amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mtoto wake.

“Kama familia tumepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mwanangu, siwezi kujua kwamba mwanangu alikuwa na ugomvi na watu wengine ama la, siku za nyuma alikua anakunywa pombe kawaida lakini hizi alizokunywa zimeondoa uhai wake. Tulimtegemea kwa kuwa alikuwa msaada kwetu, lakini tunashukuru Mungu kwa kila jambo,” amesema.

Gazeti la Mwananchi limeripoti kuwa Mjumbe wa serikali ya mtaa huo, Mohamed Mkandawile amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema Ngaga alikuwa dereva bodaboda, na kwamba shindano la kunywa pombe kali bila kupumzika ndilo limeondoa uhai wake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet