Bodaboda mbaroni kwa kumbaka abiria wake
Eric Buyanza
May 11, 2024
Share :
Huko nchini Nigeria, Polisi wa Jimbo la Ogun inamshikilia mwendesha pikipiki (Bodaboda) aliyefahamika kwa jina la Afeez Mustapha, kwa madai ya kumbaka abiria wake wa kike.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi mshukiwa huyo (Mustapha) alikuwa akimsafirisha abiria huyo lakini ghafla wakiwa njiani alibadili muelekeo na kupita njia nyingine na alipofika eneo lisilo na watu (kichakani) aliamua kumbaka.