Bodaboda waandamana kupinga maandamano ya Gen Z Kenya.
Joyce Shedrack
July 23, 2024
Share :
Kundi kubwa la madereva wa bodaboda Nchini Kenya wamejitokeza Jijini Nairobi wakiandamana kupinga maandamano ya Gen Z yaliyokuwa yamepangwa kufanyika hii leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Baadhi ya madereva hao wa bodaboda walikuwa na mabango yaliyoandikwa tunasimama na Ruto Gen Z sitisheni maandamano mpeni Rais muda wa kufanya kazi.
Hata hivyo waendesha bodaboda wa eneo la Nairobi wamewakana waandamanji hao na kuiomba serikali iache mara moja kuwatumia watu kuingilia maandamano yao.