pmbet

Bodaboda walipwa kupinga maandamano ya Gen-Z Kenya

Sisti Herman

July 24, 2024
Share :

Ripoti ya uchunguzi uliofanywa na kituo cha habari cha KTN News imebaini kuwepo kwa mashinikizo ya kisiasa kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wanaounga mkono serikali kuratibu maandamano ya kikundi cha waendesha pikipiki maarufu kama 'bodaboda' yaliyofanyika jana katikati ya jiji la Nairobi kupingana na vikundi vya vijana (Gen-Z) wanaondamana kwa wiki kadhaa sasa kupinga mambo mbalimbali yanayofanywa na serikali ya Rais William Ruto ikiwemo kupinga Muswada wa sheria ya fedha na kukithiri kwa Rushwa.

Maandamano hayo ya bodaboda waliowapinga Gen-Z yalionekana kuratibiwa na kuongozwa na mmoja ya watu waliokuwa kwenye gari aina ya Range Rover nyeusi liliobainika kuwa la mwanasiasa Mark Ndungu mmoja ya wanasiasa jijini Nairobi wanaomuunga mkono Rais Ruto.

Awali bodaboda hao walionekana kupewa maelekezo, kisha wakaelekea kwenye kituo maarufu cha mafuta kujaza mafuta ndipo walipoanza kuandamana kabla ya baadae kukutana tena pamoja huku gari lilelile likiwa pamoja nao.

Mmoja wa waandamanaji wa Gen-Z ameiambia KTN kuwa bodaboda hao walikuwa wakikwapua simu na vifaa vyao vya mawasiliano.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet