pmbet

Bodi ya Ligi yavuna faini ya Milioni 20 kwa Mnyama mechi 2.

Joyce Shedrack

March 6, 2026
Share :

Klabu ya Simba imetozwa faini ya shilingi milioni 5 kwa kosa la kuingia uwanja wa Amaan kwa mlango usio rasmi,na milioni 5 nyingine kwa kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia.

Wekundu wa msimbazi pia wametakiwa kulipa gharama za kutengeneza mlango wa chumba cha mkutano wa wanahabari.

Sambamba na hilo mnyama pia ametozwa milioni 5 nyingine kwa kosa la walinzi wake kupigana na walinzi wa Yanga kwenye mchezo wa Dabi uliofanyika New Amaan Complex.

Aidha, katika mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji Simba imetozwa faini ya shilingi milioni 5 kwa kosa la mashabiki zake kumrushia chupa mshambuliaji wa Dodoma JIJI FC, William Edgar.

Kwa mantiki hiyo klabu ya Simba italazimika kulipa jumla ya faini zote kiasi cha shilingi Milioni 20.


 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet