pmbet

Bodi ya ligi Zanzibar yataja sababu ya waamuzi kupigwa

Eric Buyanza

April 27, 2026
Share :

Kumekuwa na wimbi la waamuzi Zanzibar kushambuliwa na mashabiki wakati wa mechi, huku Bodi ya Ligi Zanzibar (ZBL) ikitaja sababu kuu inayochangia hali hiyo.
 

Akitoa ufafanuzi, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Zanzibar, Issa Kassim Ali amesema wanajitahidi kuimarisha ulinzi lakini uwanja ambao wanachezea sio rafiki kwani hauna uzio ndio maana wanashindwa kuwadhibiti mashabiki wanapoingia sehemu ya kuchezea na kufanya vurugu.
 

"Changamoto ya uwanja kutokuwa na uzio hii inatuwia vigumu kuimarisha ulinzi kwani wanaolinda ni wachache na mashabiki ni wengi, hivyo ingekuwa na uzio yasingejitokeza mambo ya aina hiyo," amesema kiongozi huyo.
 

Mtendaji huyo amesema ikitokea shabiki wa timu yoyote kumpiga mwamuzi, wanachukua sheria kwa mujibu wa kanuni za mashindano zinavyosema.

 

Kwa mujibu wa Kanuni ya 3 ya mashindano 2024-2025, kumzuia mwamuzi kufanya kazi yake ni kosa na adhabu yake ni kumfungia aliyetenda kosa hilo awe shabiki, kiongozi au mtu yeyote kufika uwanjani kwa muda maalumu na kutozwa faini isiyopungua Sh500,000 na kuendelea.
 

Mtendaji huyo amesema ikiwa shabiki atatambulika, adhabu hiyo inakwenda moja kwa moja kwake na asipotambulika klabu ndiyo itakayobeba adhabu hiyo.

 

"Tumeshafanya utekelezaji wa hilo kwa kuwafungia mashabiki, viongozi na waamuzi wanaotenda makosa, ndiyo maana pamoja na uwanja kutokuwa na uzio matukio hayo yanatokea kwa uchache kwa kuwa tunafanya utekelezaji," amesema.


 

MWANASPOTI

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet