pmbet

Bondia akataliwa na mpenzi wake ulingoni baada ya kupoteza pambano.

Joyce Shedrack

June 25, 2024
Share :

Bondia wa MMA Lukas Bukovaz,alijikuta akipoteza mapambano mawili ndani ya usiku mmoja baada ya kupokea kichapo dhidi ya mpinzani wake Jan Michalek na kudhalilika mbele ya mashabiki 20,000 baada ya kukataliwa na mpenzi wake aliyeamua kumvisha pete ulingoni.

Tukio hilo limetokea kwenye mashindano ya Clash of the Stars nchini Jamhuri ya Czech ambapo baada ya pambano kutamatika Bukovaz aliamua kumfanyia mpenzi wake surprise ya kumvalisha pete ulingoni jambo ambalo liliishia kuwa maumivu makali kwake kutokana na mpenzi wake kukataa kuvishwa pete.

Bukovaz alipiga magoti ulingoni mbele ya mpenzi wake na kuchukua kipaza sauti akamuuliza utakubali kuolewa na mimi huku akiwa ameshika pete mkononi, mpenzi wake alipokea kipaza sauti na kujibu hapana.

Mwanamke huyo aliueleza umati wa watu uliokuwa eneo hilo kwamba bondia huyo alimsaliti ndiyo sababu iliyosababisha akakataa pete yake.

Hata hivyo, bondia Bukovaz alikanusha madai hayo na kusema hajawahi kumsaliti mpenzi wake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet