Bosi wa wauza madawa ya kulevya akamatwa, ndege yake yafungwa minyororo
Eric Buyanza
July 26, 2024
Share :
Mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya duniani, Ismael "El Mayo" Zambada, anayeongoza genge llinalofahamika kama Sinaloa la nchini Mexico, amekamatwa na mawakala shirika upelelezi la Marekani Marekani katika eneo la El Paso, Texas.
Zambada, mwenye umri wa miaka 76, alianzisha genge hilo la uhalifu na Joaquin "El Chapo" Guzman, ambaye kwa sasa anatumikia kifungo nchini Marekani.
Zambada alikamatwa siku ya Alhamisi akiwa pamoja na mtoto wa kiume wa Guzman, Joaquin Guzman Lopez, ilisema wizara ya sheria ya Marekani.