pmbet

Boti ya Ambulance kujengwa Ziwa Victoria

Sisti Herman

December 24, 2023
Share :

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile jana amemwakilisha Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa jijini Mwanza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi wa ujenzi wa boti yenye vifaa vya matibabu (Ambulance Boat) ambao umesainiwa baina ya Shirika la Usalama wa Meli Tanzania (TASAC) na Kampuni ya LOCA Muhendislik Gemi ya nchini Uturuki kwa thamani ya Tsh. bilioni 4 na utatekelezwa kwa muda wa miezi 12.

 

Kihenzile amesema: “Leo nimeshuhudia utiaji saini wa kuanza kujenga hospitali inayotembea majini, ni boti ya Tsh. bilioni 4.2 itakuwa na vifaa vyote vya kisasa kwa ajili ya matibabu ya waliopata ajali majini. Spidi yake ni kilometa 30 kwa saa na inaweza kwenda umbali wa kilometa 278, ujenzi wake ambao unafanyika Ziwa Victoria, Mwanza utakamilika baada ya miezi 12.

 

“Wito wangu kwa Mkandarasi na TASAC ni kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na viwango, nimewasisitiza TASAC kuhakikisha wanaendelea na kaguzi za mara kwa mara ili kuhakikisha usalama wa usafiri huo unazingatiwa."

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet