Brahim achagua kucheza Morocco badala ya Hispania
Sisti Herman
March 11, 2024
Share :
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Brahim Diaz rasmi sasa amechagua kucheza timu ya Taifa ya Morocco badala ya Hispania ambapo amezaliwa.
Hiyo imekuja baada ya mvutano wa muda mrefu kwenye mitandao kuhusu timu ipi ya taifa atakayocheza kiungo huyo mzaliwa wa Malaga Hispania ambaye wazazi wake ni raia wa Morocco.
Shinikizo kubwa lililomshawishi kiungo huyo kuchagua kucheza Morocco ni pamoja na ushawishi wa kocha wa Morocco Walid Reagragua ambaye amemhakikishia nafasi kwenye timu yake.
Kiungo huyo mwenye uraia wa nchu hizo mbili hadi sasa akiwa na miaka 24 ameshacheza vilabu vikubwa kama AC Milan, Man City na timu ya Taifa ya Hispania ngazi za vijana.