pmbet

Brazil kukutana na Uruguay Robo Fainali Copa-America

Sisti Herman

July 3, 2024
Share :

Baada ya sare ya 1-1 Alfajiri ya leo dhidi ya Colombia, timu ya Taifa ya Brazil imefuzu hatua ya robo fainali ya kombe la Mataifa ya Amerika Kusini (Copa America) na sasa itamenyana na Timu ya Taifa ya Uruguay kwenye hatua hiyo ya mtoano.

Brazil imemaliza nafasi ya pili kwenye Kundi D alama 5 baada ya mechi tatu alama mbili nyuma ya vinara Colombia wenye pointi 7 baada ya mechi 3 ambao pia wamefuzu robo fainali ya Copa America 2024.

Katika mchezo mwingine wa Kundi D, Costa Rica waliomaliza nafasi ya tatu kwa alama nne, imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya washika mkia Paraguay wenye pointi sifuri.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet