Brazil yalazimishwa sare na Marekani
Sisti Herman
June 13, 2024
Share :
Ikiwa na maandalizi ya kombe la Mataifa ya Amerika Timu yza taifa ya Brazil na Marekani alfajiri ya leo zimecheza mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA na kumalizika kwa sare ya 1-1, Marekani ikiwa nyumbani.
Magoli ya mchezo huo yamefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Christian Pulisic kwa upande wa Marekani na mshambuliaji wa Real Madrid Rodrigo kwa upande wa Barzil.
Copa Amerika inatazamiwa kuanza kuanzia wiki ijayo huku Brazil wakiwa kundi D na timu za Costa Rica, Paraguay na Colombia huku Marekani ikiwa kundi C na timu za Bolivia, Panama na Uruguay.