Brazil yatupwa nje Copa-America na Uruguay
Sisti Herman
July 7, 2024
Share :
Timu ya taifa Brazil imeshindwa kufuzu nusu fainali ya kombe la Mataifa ya America (Copa-America) baada ya kuondolewa kwa mikwaju ya penalti 4-2 na timu ya Taifa ya Uruguay baada ya sare tasa ya 0-0 kwenye dakika za kawaida za mchezo.
Hii ni mara ya nne ndani ya misimu 6 ya michuano hiyo timu hiyo kushindwa kufuzu hatua hiyo huku ikiwa Uruguay ikifuzu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2011.
Uruguay sasa itakutana na Colomnia waliowaondoa Panama huku nusu fainali nyingine ikiwa kati Argentina dhidi Canada.