pmbet

Bridal Shower ya Chioma wa Davido awaacha watu midomo wazi.

Joyce Shedrack

June 24, 2024
Share :

Shamrashamra kuelekea harusi ya nyota wa Afrobeat kutoka Nigeria Davido pamoja na mchumba wake Chioma zinazidi kupamba moto kufuatia mambo mapya yanayoshika vichwa vya habari kujiri kila siku, usiku wa kuamkia leo huko nchini Nigeria mpenzi wa msanii huyo Chioma alifanya sherehe ya kifahari ya bridal shower iliyoacha gumzo sehemu mbalimbali kwa ukubwa wake.

Harusi hiyo inayotarajiwa kufanyika Juni 25, mwaka huu jijini Lagos nchini Nigeria na inatarajiwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri na matajiri wakubwa kutoka ndani na nje ya mipaka ya nchi hiyo.

Baadhi ya watu wakubwa wa Taifa hilo ambao wameshathibitisha kupokea mwaliko wa harusi hiyo ni mchezaji wa klabu ya Super Eagles na Napoli Victor Osimhen na aliyekuwa Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini humo Amaju Pinnick .

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet