Brighton yazikataa Bilioni 217 za Liverpool ili wamuachie Yankuba Minteh
Eric Buyanza
August 22, 2026
Share :
Ofa ya pili ya Liverpool yenye thamani ya pauni milioni 60 (sawa na shilingi Bilioni 217 za kitanzania) kwa ajili ya kumsajili mchezaji Yankuba Minteh wa Brighton imekataliwa.
Taarifa za uhakika zinasema kuwa Brighton wamegomea kiasi hicho. Hii imekuja siku moja tu baada ya ofa ya kwanza ya pauni milioni 50 kukataliwa pia.
Brighton wanashikilia msimamo kuwa wanataka £70 milioni ili wamuuze winga huyo mwenye umri wa miaka 22.






