Brock Lesnar atangaza kustaafu baada ya kutandikwa na Mnigeria
Eric Buyanza
August 5, 2026
Share :
Brock Lesnar ametangaza kustaafu rasmi mchezo wa mieleka baada ya kupigwa Jumamosi usiku na kijana mwenye asili ya kinigeria, Oba Femi.
Akiwa kwenye kipindi cha *The Pat McAfee Show* jana siku chache baada ya tukio hilo, Lesnar aliweka wazi kuwa pambano hilo dhidi ya Oba Femi ndilo lililokuwa la mwisho.
"Niko hapa leo kufanya mahojiano haya ili dunia na kila mtu wafahamu kuwa nimestaafu, na nilitaka kutoa shukrani za dhati kwa kila mtu. Jumamosi ilikuwa siku yenye hisia kali sana kwangu,"
"Oba Femi aliponitupa chini kwa nguvu katika *WrestleMania*, nilijisemea........ Huo ndio mwisho wangu ndani ya ulingo" alisema Lesnar.






