Bruno ampa Salute Carrick
Sisti Herman
February 8, 2026
Share :

Bruno Fernandes amesifu mchango na uwezo wa kocha mkuu, Michael Carrick baada ya Manchester United kushinda mechi nne mfululizo tangu kiungo huyo wa zamani wa klabu hiyo achukue usukani hapo Old Trafford.
Man United ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Tottenham Hotspur Jumamosi na kuongeza mwanzo mzuri wa ushindi wa Carrick wa asilimia 100 kama kocha mkuu na kuongeza matumaini ya kurudi Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kukosa nafasi hiyo kwa miaka miwili iliyopita.
"Michael ameshinda kila kitu hapa na anajua inamaanisha nini kwa mashabiki hawa. Inamaanisha nini kwa klabu kushinda na ni kiasi gani kinachohitajika kushinda katika klabu hii ya mpira wa miguu.
Nadhani hiyo inaongeza kitu maalum kwa timu," alisema nahodha huyo wa United akiiambia TNT Sports.





