Bukayo Saka kulamba mkataba wa muda mrefu Emirates
Eric Buyanza
April 1, 2025
Share :
Winga wa Arsenal na timu ya taifa ya England, Bukayo Saka, ataingia katika mazungumzo mapya ya mkataba, huku mkurugenzi mpya wa michezo wa Arsenal, Andrea Berta, akitaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 asaini mkataba wa muda mrefu.
Andrea Berta, ambaye hivi majuzi alichukua nafasi ya mkurugenzi wa michezo, atakuwa na jukumu la kusimamia uboreshaji wa kandarasi ya Saka.
Bukayo kwa sasa anapokea Pauni laki 195 kwa wiki, alisaini mkataba wake wa mwisho mwaka 2022.
Arsenal leo Jumanne watawakariibisha Fulham kwenye Uwanja wa Emirates kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa majira ya saa 3:45 Usiku.