Bunge la Tanzania latakiwa kuwa na uwiano sawa kwa wanawake na wanaume
Eric Buyanza
March 6, 2024
Share :
Kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani March 8, Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP unahimiza usawa wa kijinsia katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na maeneo yote ya uongozi nchini ili kuwepo na maamuzi ya kitaifa yenye kujali ustawi wa jansia zote mbili.
TGNP inasema licha ya Bunge la Tanzania kupata Spika wa Bunge mwanamke kwa awamu 2 lakini bado idadi ya wabunge wanawake ni ndongo ikilinganishwa na wabunge wanaume.
Wabunge wanawake ni 141 huku wanaume wapo 393 idadi ambayo haiakisi lengo la asilimia 50 kwa amsini 50
"Idadi ya wanawake ni 24 kati ya Wabunge 264 ambayo ni sawa na asimilia 9.1, idadi ya Wabunge wanawake wa viti maalumu ni 113 ambayo ni sawa na asilimia 29 ya wabunge wote.
Jumla ya wabunge wanawake ni 141 sawa na asilimia 37 ya wabunge wote ambao ni 393.
Hii bado ni idadi ndogo ukilinganisha na lengo la kufikia asilimia 50 kwa 50" amesema Mkurugenzi wa TGNP Bi. Lilian Liundu