Burkinaso, Mali na Niger zajitoa Ecowas
Sisti Herman
January 28, 2024
Share :
Burkina Faso, Mali na Niger, zimetangaza Jumapili hii, Januari 28 kujiondoa mara moja kwenye Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS),tangazo ambalo limetangazwa kwenye vituo vya Televisheni vya umma vya nchi hizo tatu.
Taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari imesainiwa na Assimi Goïta wa Mali, Ibrahim Traoré wa Burkina Faso na Abdourahamane Tiani wa Niger.
Mojawapo ya sababu za kujiondoa ECOWAS ni ukosefu wa uungwaji mkono katika mapambano dhidi ya ugaidi na kuwekewa vikwazo vya kiuchumi kwa nchi hizo.