pmbet

Burna Boy aacha balaa Uingereza baada ya Show yake.

Joyce Shedrack

July 5, 2024
Share :

Staa wa muziki wa Nigeria Burna Boy amezua gumzo Nchini Uiengereza na Duniani kote baada ya show yake aliyoifanya siku ya jumamosi katika uwanja wa London Stadium wenye uwezo wa kubeba watu 80,000 na kujaza uwanja huo.

Burna Boy ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika kujaza uwanja huo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya show yake ya kwanza miaka kadhaa iliyopita na kujaza uwanja huo.

Msanii huyo ambaye ni mshindi wa tuzo za Grammy anaitaja Uingereza kama mji wake wa nyumbani na aliwahi pia kufanya kolabo na wasanii kama Ed Sheeran, Jorja Smith, Coldplay’s Chris Martin, Lily Allen na wengine wengi.

Burna Boy yupo kwenye ziara ya kutangaza album yake ya mwisho ya 'I Told Them' ziara ambayo atazunguka Nchi mbalimbali barani Ulaya kwa ajili ya kufanya Show.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet