Burna Boy apiga mweleka na kuanguka akiwa stejini
Eric Buyanza
July 29, 2024
Share :
Nyota wa muziki wa AfroBeat kutoka Nigeria, Burna Boy, ameanguka wakati akitumbuiza jukwaani.
Tukio hilo lilitokea wakati akiwa kwenye tamasha la kumbukumbu ya albamu yake ya tatu ya (African Giant).
Akiwa amepandwa na mzuka msanii huyo aliruka kutoka stejini na kukanyaga spika akijaribu kuelekea kwa mashabiki na ndipo alipopiga mweleka na kuanguka chini kabla ya kwenda kuokolewa na mabaunsa.
Hata hivyo msanii huyo hakuumia na aliendelea na tamasha.