Burna Boy; Hakuna msanii anayeweza kuandika nyimbo ya hadhi yangu
Sisti Herman
July 7, 2024
Share :
Msanii wa muziki wa Nigeria BurnaBoy amedai kuwa hakuna mwandishi wa nyimbo anayeweza kuandika wimbo unaoendana na ukubwa wake.
Burna Boy ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa X (zamani Twitter) ambapo ameandika kuwa jina lolote linaloonekana katika nyimbo zake kama Pruducer au msanii aliyemshirikisha hawezi kuwa mwandishi wake.
Hata hivyo kupitia maandiko hayo ameleeza kuwa kuna muda mataifa ya Magharibi huweka watayarishaji kama waandishi wa ngoma na kuweka majina yao kwenye nyimbo kama waandishi huku akidai kwa upande wake hakuna anayeweza kuandika wimbo wa hadhi yake.
Hayo ni baada ya msanii Logos Olori ambaye kwa sasa anamtungia nyimbo Davido, kudau kuwa siyo bosi wake tu anayetungiwa nyimbo bali Wizkid, Burna Boy na wasanii wengine wakubwa wanatumia watunzi wa nyimbo.