Burna Boy kufanya show live usiku wa Grammy
Sisti Herman
January 22, 2024
Share :
Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Burna Boy anatarajia kutumbuiza kwenye sherehe ya ugawaji tuzo za Grammy 2024 zitakazofanyika Februari 4 katika ukumbi wa Crypto mjini Los Angeles nchini Marekani.
Burna Boy anaweka historia kuwa msanii wa kwanza kutoka Nigeria kutumbuiza katika tuzo za Grammys ambapo mwaka 2021 aliwahi kushinda tuzo hizo katika kipengele Albamu bora ya muziki wa Grobal ‘Destiny’.