pmbet

Burna Boy mwanaume mwenye mvuto zaidi Afrika

Sisti Herman

April 14, 2024
Share :

Jarida la mitindo la 'Essence' la nchini Marekani limemtaja nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria kwenye orodha ya mastaa wa kiume wanaovutia zaidi duniani.

Kwa mujibu wa Mhariri wa jarida hilo, Rivea Ruff, staa huyo wa Afro Beats ameingia kwenye orodha hiyo kutokana na mwili wake kuwa wa kuvutia zaidi, mitindo yake tofauti ya Kiafrika pamoja na sauti yake inayowavutia mashabiki akiwa jukwaani.

Orodha hiyo ya Essence ‘Sexiest Men Of The Moment’, inaongozwa na mwigizaji wa Uingereza Damson Idris, huku mastaa wengine walioingia katika listi hiyo akiwemo Usher, Colman, Trevente Rhodes, Daniel Kaluuya na Skepta.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet