Burna boy ndiye msanii namba moja wa Nigeria - 2Face
Eric Buyanza
September 3, 2025
Share :
Kutoka nchini Nigeria, mwanamuziki mkongwe Innocent Idibia, maarufu kwa jina la 2Face au 2Baba, amemtangaza Burna Boy kama msanii namba moja wa Nigeria kwa sasa.
2Face anamuelezea Burna Boy kama kiongozi na "mwandamizi" wa mazao ya sasa ya wasanii wa Nigeria.
"Kwa kiwango binafsi, Burna Boy ndiye namba moja wangu. Ingawa bado nina wasanii wengine ninaowakubali. Lakini mimi binafsi nikiwa msanii Burna Boy ndiye namba moja kwa sasa. Kati ya hao wote ninaowataja yeye ndiye mkubwa.”
"Bado kuna wengine wanakuja nyuma yake ambao naona wanaenda kwa kiwango sawa," 2Face alisema.