Burna boy, Wizkid, Davido wamuacha Diamond mbali kwa kulipwa
Eric Buyanza
March 13, 2024
Share :
Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na jarida la 'African Fact Zone', wasanii wa Tanzania, Diamond Platnumz, Ali Kiba, Harmonize na Rayvanny ndio wanaoongoza kwa kulipwa pesa nyingi kwenye onyesho moja.
Katika orodha hiyo, Diamond ametajwa kulipwa hela za kitanzania Shilingi (milioni 250), Kiba (milioni 100), Harmonize (milioni 50) na Rayvanny (milioni 40).
Katika Jarida hilo pia wametajwa wasanii wa Nigeria Burna Boy, Wizkid, Rema na Davido kama vinara wa kulipwa pesa ndefu zaidi.
Wanigeria hao kila mmoja anapokea $ milioni moja kwa show, sawa na shilingi Bilioni 2.5 za kitanzania.