pmbet

Burudani ya Dar Port Kagame Cup kutamatika hii leo.

Joyce Shedrack

July 21, 2024
Share :

Michuano ya Dar Port Kagame Cup 2024 inatamatika hii leo kwa kupigwa michezo miwili mmoja wa Fainali kati ya APR FC ya Rwanda na Red Arrows ya Zambia  huku mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya Al hilal ya Sudan na AL Wadi Fc zote za Sudan.

 

Fainali ya michuano hiyo itapigwa majira saa 9:00 alasiri kwenye uwanja wa KMC, bingwa wa Ligi Kuu nchini Rwanda APR akisaka taji lake la  nne katika michuano hiyo iliyodhaminiwa na Rais wa Nchi yao, Paul Kagame.

APR ilitinga fainali ya michuano hiyo baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Al Hilal ya Sudan   baada ya dakika 120 kumalizika bila bao lolote kwa timu zote mbili, Red Arrows walifanikiwa kutinga fainali baada ya kuwafunga Al Wadi  ya Sudan mabao 2-0 katika mchezo wa nusu fainali.

Mashindano hayo yalianza Julai 9 yakishirikisha timu 12,Tanzania ikitoa timu mbili pekee ambazo ni Coastal Union na Singida Black Stars ambazo zote zilitupwa nje ya mashindano hayo. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet