pmbet

Burundi kuwapokea wahamiaji wanaotimuliwa marekani

Eric Buyanza

October 1, 2026
Share :

Serikali ya Burundi imethibitisha rasmi kukubali kuwapokea raia wa kigeni na wahamiaji wanaofukuzwa kutoka nchini Marekani, ikiwa ni sehemu ya mikataba mipya inayotekelezwa chini ya sera kali za uhamiaji za serikali ya Washington.

 

Burundi inakuwa nchi ya hivi karibuni barani Afrika kusaini makubaliano hayo na serikali ya Rais Donald Trump, ambapo nchi hiyo itapokea hata wahamiaji ambao si raia wake wa asili (third-country deportees).
Akizungumza kuhusu uamuzi huo, Msemaji wa Rais wa Burundi, Nancy Ninette Mutoni, amesema kuwa nchi hiyo iko tayari kuwapokea watu hao, lakini akaweka wazi masharti magumu yaliyowekwa na Bujumbura.

 

"Tutapokea tu wale ambao hawana rekodi za uhalifu na wasio na uhusiano wowote na makundi ya kigaidi," alisema Mutoni. Aliongeza kuwa wahamiaji watakaowasili watapewa fursa ya kuomba uraia wa Burundi iwapo watakidhi vigezo vya kisheria na kuonesha nia ya kuchangia maendeleo ya taifa hilo.

Hata hivyo, serikali ya Burundi haijaweka wazi idadi kamili ya wahamiaji watakaopokelewa, tarehe rasmi ya kuwasili kwao, wala kiasi cha fedha ambacho Marekani itazilipa mamlaka za Burundi kufanikisha mpango huo.

 

Msemaji huyo alibainisha kuwa taratibu za ndani zimeshaanza kuratibiwa ili kupanga maeneo watakayoishi, mahitaji yao ya chakula, na namna watakavyounganishwa kwa usalama na jamii ya wenyeji.

Kwa uamuzi huu, Burundi inaungana na mataifa mengine zaidi ya 10 barani Afrika—ikiwemo nchi jirani ya Rwanda, Uganda, Sudan Kusini, Eswatini, na Ghana—ambayo tayari gametangia makubaliano na Marekani kupokea watu wanaofukuzwa.

 

Licha ya serikali hizi kuona makubaliano hayo kama fursa ya kidiplomasia na kiuchumi, mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu yameendelea kukosoa vikali mpango huo, yakidai kuwa unakiuka sheria za kimataifa zinazolinda haki na usalama wa wahamiaji na wanaotafuta hifadhi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet