Burundi yafunga mipaka yake na Rwanda
Sisti Herman
January 12, 2024
Share :
Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia taarifa kwa vyombo vya habari limeeleza kuwa kwasasa hakuna Mwananchi anayeruhusiwa kuvuka kutoka Burundi kwenda Rwanda halikadhalika kwa wanaotoka Rwanda kuelekea Burundi.
Hatua hiyo imekuja baada ya hivi karibuni viongozi nchini Burundi kuishutumu Rwanda kwa kuwaficha waasi dhidi ya Serikali ya Rais Evariste Ndayishimiye.
Kwa mjibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani Martin Niteretse,hakuna atakayeruhusiwa kutumia mipaka ya Rugomba mkoani Cibitoke na Ruhwa mkoani Ngozi mpaka pale hatua nyingine zitakapochukuliwa.
Uhusiano kati ya Burundi na Rwanda ulikuja kuingia doa mwaka wa 2015 baada ya kutokea kwa jaribio la mapinduzi ambalo lilifeli baadae, Burundi ikiwashutumu kuwaficha washukiwa hao.