pmbet

CAF wametupa VAR - Karia

Sisti Herman

December 16, 2023
Share :

Rais wa shirikisho la soka nchini (TFF) Wallace Karia amethibitisha kuwa mahusiano mazuri waliyoyajenga na mashirikisho ya kimataifa ya mchezo huo yameanza kuzaa matunda baada ya shirikisho la soka barari Afrika (CAF) kuisaidia TFF kuweka teknolojia ya kuwasaidia waamuzi kwa njia ya video (VAR) kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

 

“Mbali na mahusiano na mashirikisho kama Morocco na Saudi Arabia lakini pia mahusiano yetu na CAF, na hapa naomba niwatangazie rasmi tumepata VAR ambayo itakuwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, wataalamu wameingia jana, watatoa mafunzo kwa waratibu wetu na tutaangalia pia kupitia mahusiano na mashirikisho mengine watusaidie kufikia daraja hilo, mfano hivi sasa pia tunahangaika uwanja wa Amani pia uwe na VAR” alisema Karia

 

Karia amesema hayo kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa TFF unaofanyika mjini Iringa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet