CAF waongeza zawadi AFCON
Sisti Herman
January 4, 2024
Share :
Shirikisho la soka Barani Afrika “CAF” leo limetangaza ongezeko la asilimia 40 ya pesa atakayochukua bingwa wa mashindano ya AFCON 2023 nchini Ivory Coast.
Bingwa wa michuano ya AFCON kwasasa ataondoka na kitita cha USD 7,000,000.
Mshindi wa pili katika michuano hiyo ataondoka na USD 4,000,000.
Timu zote zitakazofika hatua ya nusu fainali ya mashindano haya zitapokea USD 2,500,000.
Timu zote nane zitakazofika hatua ya robo fainali zitapokea USD 1,300,000.
Rais wa shirikisho la soka Barani Afrika “CAF” Patrice Motsepe ametangaza ongezeko la zawadi hizo.