CAF yaridhshwa na kasi ya maandalizi ya AFCON 2027
Sisti Herman
November 1, 2026
Share :

Katika kuendelea kujiandaa na mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) leo Oktoba 31, 2026, limefanya ukaguzi wa miundombinu ya viwanja vitakavyotumika katika jiji la Dar es Salaam, ikiwemo Uwanja wa Benjamin Mkapa pamoja na viwanja vya mazoezi.
Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Katibu Mkuu wa CAF, Bw. Samson Adamu, amesema kuwa Shirikisho hilo limeridhishwa na maendeleo ya viwanja vya mazoezi na ukarabati wa miundombinu unaoendelea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Ameeleza kuwa CAF ina imani kubwa kuwa maandalizi yanayoendelea yatawezesha mashindano ya AFCON 2027 kufanyika nchini Tanzania kwa ubora na viwango vya juu vya kimataifa.





