Calafiori awahi Uingereza kwa vipimo, kujumuishwa ziara ya Marekani
Eric Buyanza
July 26, 2024
Share :
Beki wa Bologna, Riccardo Calafiori, anaelekea Uingereza leo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya na Klabu ya Arsenal.
Calafiori yuko mbioni kusajiliwa na The Gunners baada ya kukubali ada ya Pauni milioni 42.1 (sawa na Bilioni 146 za kibongo).
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia, ambaye aling'ara kwenye michuano ya Euro 2024, atajiunga na kikosi cha Mikel Arteta kwa ajili ya ziara yao ya nchini Marekani.