Camara na Diarra kuchuana na Mendy tuzo za Afrika Magharibi.
Joyce Shedrack
May 29, 2025
Share :
Golikipa wa klabu ya Simba Moussa Camara na golikipa wa klabu ya Yanga Djigui Diarra ni miongoni mwa walinda milango waliochaguliwa kuwania tuzo ya kipa bora wa Afrika Magharibi kwa msimu wa 2024/25.
Magolikipa hao kutoka klabu za Kariakoo wanaungana na Edouard Mendy wa Al-Ahli ya Saudi Arabia,Yahia Fofana kutoka klabu ya Angers na Youssouf Koita wa Djoliba Ac ya Mali.