Camara na Diarra vita ya Clean Sheet yapamba moto
Sisti Herman
April 25, 2025
Share :
Vita ya kuwani tuzo ya kipa bora wa msimu wa Ligi kuu Tanzania bara licha ya kwamba imemsogelea zaidi kipa wa klabu ya Simba Moussa Camara, lakini kipa wa klabu ya Yanga Djigui Diarra naye hakai mbali kwenye ushindani huo kwani hadi sasa wametofautiana hatisafi (clean sheet) moja tu, huku Simba wakiwa na michezo minne mkononi.
Hadi sasa kwenye Ligi kuu hii ndiyo orodha ya makipa wanaoongoza kwa Clean Sheets;
1. Moussa Camara (Simba) - 15
2. Djigui Diarra (Yanga) - 14
3. Patrick Munthali (Mashujaa) - 12
4. Mohamed Mustapha (Azam) - 10
5. Yona Amos (Pamba) - 9
Je unadhani nani ataibuka shujaa mwisho wa msimu?