pmbet

Cameroon ya sasa sio kama ya zamani - Song

Sisti Herman

January 21, 2024
Share :

Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya Cameroon Rigobert Song ameweka wazi kuwa kwasada Cameroon ipo kwenye ujenzi na watu wasiiringanishe na ile Cameroon ya zamani.

 

Song ameyazungumza hayo baada ya kupoteza mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya Senegali [3-1] na kusisitiza kuwa wana nafasi ya kusonga mbele kwenye hatua inayofuata.

 

“Lazima tutambue kwamba Cameroon ya sasa haipo kama ilivyokuwa zamani”.

 

“Bado tunajenga timu yetu kwaajili ya siku zijazo, hata kama mimi nitaondoka ila atakayenifuata ahakikishe anatengeneza timu nzuri”.

 

“Pamoja na hilo, Binafsi naamini tutafuzu hatua inayofuata, bado tuna nafasi”, alisema Rigobert Song Kocha mkuu wa Cameroon.

 

Cameroon kwasasa ina alama moja baada ya kutoka sare kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Guinea, kundi hilo linaongozwa na Senega [6], Guinea [4], Cameroom [1], na Gambia [0].

 

Mchezo unaofuata kwa Cameroon ni Jumanne January 23, dhidi ya Gambia majira ya saa mbili [20:00] usiku na huu ndio mchezo utakaotoa hatma ya Cameroon kwenye michuano hii.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet