Canada yasema kikosi maalumu cha Jeshi la Iran ni cha kigaidi
Eric Buyanza
June 20, 2024
Share :
Canada imekiorodhesha kitengo chenye ushawishi mkubwa cha jeshi la mapinduzi la Iran, Islamic Revolutionary Guard Corps (IRGC), kama kundi la kigaidi.
Waziri wa Canada anayeshughulikia masuala ya usalama wa umma, Dominic LeBlanc, amesema hatua hiyo inatoa ujumbe mzito kwamba Canada itatumia zana zote ilizonazo kupambana na kundi hilo la kigaidi.
Waziri huyo aidha amesema serikali ya Canada itahakikisha kwamba hakuna kinga yoyote kwa hatua zisizo halali za Iran na msaada wake kwa ugaidi.
Uamuzi huo una maana, pamoja na mambo mengine, kwamba ni kosa la uhalifu kwa mtu yoyote nchini Canada kukipatia msaada wa fedha au vifaa kitengo hicho cha jeshi la Iran na kwamba mali zake nchini humo zinatakiwa zizuiwe.
Waziri wa mambo ya nje wa Israel Israel Katz ameipongeza hatua hiyo.