Cape Verde yatangazwa nchi ya tatu Afrika kutokomeza Malaria
Eric Buyanza
January 15, 2024
Share :
Shirika la Afya Duniani (WHO), limeitangaza Cape Verde kuwa nchi ya tatu barani Afrika kutokomeza ugonjwa wa Malaria, wakati ambapo ugonjwa huo bado unaendelea kuwaua maelfu ya watu barani huu.
Mkurugenzi wa shirika la afya duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amekipongeza kisiwa hicho kwa ustahimilivu katika safari yake ya kutokomeza maradhi hayo.
Kisiwa hicho chenye wakaazi wapatao laki tano kinafuatia nchi za Mauritius na Algeria ambazo zimetangazwa kudhibiti Malaria. Duniani kote, nchi takribani 43 zimeorodheshwa na WHO kudhibiti ugonjwa huo.