Capt. Traore apiga marufuku ndoa za jinsia moja Burkina Faso
Sisti Herman
April 21, 2025
Share :
Rais wa serikali ya kijeshi ya Burkina Faso Capt. Ibrahim Traore rasmi amepiga marufuku kufungwa kwa ndoa za jinsia moja nchini humo na kubainisha wazi kuwa watakaobainika kufunga na kufungisha watashtakiwa kwa mujibu wa sheria inayoambatana na adhabu kali.
"Yeyote atakayekamatwa akishiriki kufunga au kufungisha ndoa za jinsia moja watakumbana na mkono wa sheria kwasababu haziendani na tamaduni za Afrika"
Hiyo ni nukuu ya Traore kama ilivyonukuliwa na Afrika World.