pmbet

Capt. Traore kutua Tanzania wiki ijayo

Sisti Herman

January 23, 2025
Share :

Rais wa Bukina Faso, Capt. Ibrahim Traoré ni miongoni mwa marais 25 watakaoshiriki mkutano wa nishati uliopangwa kufanyika Dar es Salaam Januari 27 na 28 mwaka huu.

Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia masuala ya nishati na mabadiliko ya hali ya hewa, Dk Kevin Kariuki amesema pia mawaziri wa fedha na nishati 60 wa Afrika watashiriki mkutano huo.

Aidha, viongozi wengine wa kimataifa watashuhudia wakuu wa nchi za Afrika wakikubaliana kusaini Mpango Mahususi wa Nishati wa Afrika, awamu ya kwanza utakaozishirikisha nchi 14. Nchi hizo ni Tanzania, Malawi, Chad, Nigeria, Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Niger, Liberia, Msumbiji, Madagascar, Zambia, Mali, Ivory Coast na Mauritania.

Alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano huo unadhaminiwa na Benki ya Dunia, AfDB na washirika wengine wa maendeleo kuhakikisha watu milioni 300 Afrika wanafikiwa na umeme ifikapo mwaka 2030.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet