Cardi B afurahishwa Kamala Harris kuwa mgombea Urais
Eric Buyanza
July 22, 2024
Share :
Rapa mtata wa Marekani Cardi B, ameunga mkono Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris kuwa mgombea wa chama cha Democrat katika uchaguzi wa urais wa Marekani utakaofanyika November mwaka huu.
Cardi B ambaye siku za nyuma aliwahi kutoa maoni yake akisema kwamba Bi Harris anafaa kuwa mgombea wa Chama cha Democrat, alizikaribisha kwa msisimko habari za Biden kujiuzulu kugombea kiti hicho hapo jana.
Kupitia mtandao wake wa X (zamani Twitter), Cardi B aliandika: “Aha hahaha Niliwaambia Kamala [Harris] alipaswa kuwa mgombea wa 2024… Msicheze na mimi!”
Akiongea na tovuti ya Rolling Stone mwezi Mei, Cardi B aliahidi kutopiga kura katika uchaguzi wa Novemba ikiwa wagombea wangeendelea kuwa Rais wa sasa Joe Biden wa Chama cha Democrat, na Donald Trump wa Chama cha Republican.