Cardi B amzalia mpenzi wake mpya kabla ya talaka na aliyekuwa mumewe.
Joyce Shedrack
September 18, 2025
Share :
Rapa Cardi B amefanya maamuzi ya kumzalia mpenzi wake Mpya Stefon Diggs kabla hata talaka yake na aliyekuwa mume wake ambae ni Offset kumalizika kutolewa.
Kupitia mahojiano ambayo Cardi B aliyoyafanya hivi karibuni ameweka wazi kuwa anatarajia mtoto wake wa nne kabla ya mwezi Februari 2026 huku akiendelea na shughuli zake za kimuziki kama kawaida.
Cardi B tayari ni mama wa watoto watatu Kulture, Wave, na Blossoms huku Mpenzi wake Stefon Diggs akiwa tayari ni baba wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Nova.