Cardi B ashtakiwa kisa ngoma yake ya 'Enough'
Joyce Shedrack
July 5, 2024
Share :
Msanii wa muziki kutoka Marekani Cardi B ameshitakiwa na wasanii wawili nchini hiyo Joshua Fraustro na Miguel Aguilar maarufu kama Kemika 1956 kwa madai ya kutumia baadhi ya mistari yao katika wimbo wake wa ‘Enough’ bila kuwapa taarifa.
Wasanii hao wamedai kuwa Cardi B na watayarishaji wake walitumia vipengele vya wimbo wao wa mwaka 2021 "Greasy Frybread" katika wimbo wa rapa huyo maarufu uliotoka mwaka huu .
Kemika 1956 wamefungua mashtaka hayo dhidi ya Cardi B, OG Parker ambaye ni producer wa msanii huyo, DJ SwanQo ,kampuni ya Atlantic Records na Warner Music Group walioandaa na kuruhusu wimbo huo utoke wakitaka kulipwa fidia ya Dola 50 milioni.
Machi 15 mwaka huu ndiyo tarehe ambayo Cardi B aliiachia ngoma hiyo na kufanya vizuri Nchini humo hadi kuingia kwenye orodha ya hits 10 bora nchini humo.